Klabu ya Simba SC imepigwa faini ya dollar za Kimarekani Dollar 50,000 sawa na Tsh 135,000,000 na kutakiwa kucheza bila mashabiki mchezo ujao wa CAF Champions League dhidi Gaborone Unitedya Botswana utakaochezwa.
Inaelezwa sababu au chanzo cha klabu hiyo kuingia bila mashabiki kwenye mchezo huo wa CAF Champions League ni kutokana na tukio la mchezo wa Kombe la Shirikisho msimu uliopita dhidi ya Al Masry ya Misri, ambapo mashabiki kuingia uwanjani na mabomu ya moshi na kuwasha mafataki (moto) kwenye mchezo huo wa robo fainali ambao walishinda.
Kwa matokeo hayo, mchezo wa Simba dhidi ya Gaborone United (Botswana) katika Uwanja wa Benjamin Mkapa utachezwa bila mashabiki, hakuna kuruhusiwa watazamaji.
CAF pia imeweka marufuku ya mechi mbili za nyumbani:
• Moja itatekelezwa sasa.
• Ya pili iko kwa masharti, itatekelezwa endapo kutatokea tukio la utovu wa nidhamu tena msimu huu.
Muhimu: Hakuna adhabu yoyote iliyotolewa kutokana na fainali dhidi ya RS Berkane, kinyume na baadhi ya taarifa zinazoenezwa.
Baada ya adhabu hiyo klabu ya Simba SC imefanya juhudi za kukata rufaa kupinga maamuzi hayo ya kamati nidhamu ya CAF lakini hawapati ushirikiano sahihi ikiwa viongozi wanaendelea kupambana kukata rufaa hiyo.
#Anoldmathias255✍🏾

Hakuna maoni:
Chapisha Maoni