Breaking


Jumatano, 3 Septemba 2025

TCU YAFUNGUA DIRISHA LA UDAHILI AWAMU YA PILI

TUME ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU), imefungua dirisha la udahili awamu ya pili kwa wanafunzi wa shahada ya kwanza kwa mwaka wa masomo 2025/2026 kuanzia leo hadi Septemba 21, mwaka huu.

 Hatua hiyo imetokana na kukamilika kwa awamu ya kwanza ya udahili huo,  ambapo waombaji 116,596 sawa na asilimia 79.4 ya waombaji wote waliiomba wamepata udahili katika vyuo walivyoomba.

Pia, imesema waombaji waliodahiliwa katika chuo zaidi ya kimoja wanapaswa kuthibitisha udahili wao chuo kimojawapo kuanzia leo hadi Septemba 21, mwaka huu.

Katibu Mtendaji wa TCU, Profesa Charles Kihampa, amesema hayo jijini Dar es Salaam, leo alipozungumza na waandishi wa habari kuhusu kukamilika kwa awamu ya kwanza na kufunguliwa kwa awamu ya pili ya udahili wa shahada ya kwanza kwa mwaka wa masomo 2025/2026.

Aidha, TCU imevielekeza vyuo vya elimu ya juu nchini kutangaza programu ambazo bado zina nafasi na waombaji wa udahili na vyuo kuzingatia utaratibu wa udahili wa awamu wa pili kama ilivyooneshwa katika kalenda ya udahili iliyopo tovuti ya TCU.

Hakuna maoni: