Marc Guehi hajafurahishwa sana na Crystal Palace kwa kumnyima uhamisho wa £35m kwenda Liverpool, ambayo ilikuja baada ya meneja Oliver Glasner kutishia kujiuzulu ikiwa beki huyo wa Uingereza mwenye umri wa miaka 25 atauzwa. (Guardian)
Kama Liverpool wangetoa pauni milioni 55 kwa Guehi basi Crystal Palace wangeendelea na uhamisho huo na huenda Reds wakakabiliwa na ushindani kutoka kwa Real Madrid kumsajili bila malipo. (Telegraph – Subscription Required)
Guehi, katika mwaka wa mwisho wa kandarasi yake ya Crystal Palace, atakataa ofa yoyote ya mkataba mpya huku akipanga kuondoka kama mchezaji huru msimu ujao wa joto. (Time – Subscription Required)
Manchester United ilitaka kumnunua tena Danny Welbeck kutoka Brighton kwa mwaka wa pili msimu huu wa joto, lakini mmiliki mwenza Sir Jim Ratcliffe hakuidhinisha uhamisho wa mshambuliaji huyo wa zamani wa Uingereza mwenye umri wa miaka 35. (Athletic – Subscription Required)
#ChanzoBbcswahili

Hakuna maoni:
Chapisha Maoni