Breaking


Ijumaa, 26 Septemba 2025

TUNAENDA KUJENGA KIZAZI CHENYE MAADILI KWA KUTUMIA TEKNOLOJIA-RAIS SAMIA


MGOMBEA wa nafasi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama Cha Mapindizi(CCM),Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan,amesema miaka mitano ijayo serikali yake inaenda kujenga kizazi kijacho chenye maadili kwa kutumia teknolojia ambazo hazitakiuka utamaduni wa mtanzania na kuharibu watoto.

Rais Samia amesema hayo Septemba 26,2025,wakati wa mkutano wa kampeni uliofanyika Uwanja wa Sabasaba uliopo Mtwara Mjini Mkoani Mtwara.

Amesema miaka mitano ijayo itakuwa ya kupiga hatua kwenye teknolojia za kisasa,kudumisha mila na desturi zile zenye ubora.

"Tutaongeza matumizi ya teknolojia ya kisasa ikiwemo akili unde katika kutoa huduma na kwa sasa tumeanza kwenye kilimo,"amesema

Hakuna maoni: