Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo na Msemaji Mkuu wa Serikali, Ndg. Gerson Msigwa, amekabidhi kiasi cha shilingi milioni arobaini na tano (45,000,000/=) kwa timu ya Azam FC kama zawadi ya “Goli la Mama” kutoka kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Zawadi hiyo imetolewa kama pongezi kwa Azam FC baada ya kuibuka na ushindi mnono wa mabao 7-0 dhidi ya KMKM ya Zanzibar katika mchezo wa marudiano wa michuano ya Kombe la Shirikisho la Afrika (CAF Confederation Cup), uliochezwa jijini Dar es Salaam.
Azam FC pia walipata ushindi wa mabao 2-0 kwenye mchezo wa kwanza uliochezwa Zanzibar, na hivyo kufanikiwa kusonga mbele kwa jumla ya mabao 9-0, hatua ambayo imewapeleka rasmi kwenye makundi ya Kombe la Shirikisho la Afrika.
#Official-Isharoja✍🏾






Hakuna maoni:
Chapisha Maoni