Naibu Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi(CCM), Zanzibar Dk.Mohammed Said Mohammed ‘Dimwa’ amesema ilani ya uchaguzi mkuu wa CCM ya mwaka 2025/2030 imelenga Zaidi katika mikakati endelevu ya kuongeza ajira kukuza uchumi wa buluu.
Kauli hiyo ameitoa wakati akizungumza kwenye mkutano wa kampeni unaofanyika uwanja wa Bumbwini uliopo wilaya ya Kaskazini B mkoa wa Kaskazini Unguja.
Naibu Katibu Mkuu huyo amesema katika kipindi cha miaka mitano serikali itajikita katika kuimarisha huduma za kijamii na kuhakikisha kila mwananchi wa Zanzibra anafaidikana matunda ya mapinduzi.
“Kwa msingi huo ni jukuu letu sote wananchi wa jimbo la Bumbwini kuhakikisha kwamba Oktoba 29 mwaka huu tunajitokeza kwa wingi kuwapigia kura wagombea wetu wa CCM,ili safari hii ya maendeleo iendelee na ahadi zilizomo kwenye ilani yetu zitekelezwe,”amesema

Hakuna maoni:
Chapisha Maoni