Breaking

Jumanne, 21 Oktoba 2025

MAMIA YA WAFANYABIASHARA KAGERA WAJITOKEZA KUPATA ELIMU YA KODI

 

Wafanyabiashara zaidi ya 1000 wa  Mkoani Kagera wamejitokeza kwa ajili ya kupata elimu ya kodi mbalimbali na kujifunza umuhimu wa dawati maalumu la uwezeshaji biashara katika kukuza biashara zao. 

Elimu hiyo imetolewa tarehe 20.10.2025  katika Semina iliyoandaliwa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kwa wafanyabiashara wadogo na wajasiriamali wa Mkoa wa Kagera ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa mipango ya TRA kuwafikia walipakodi na kuwapa elimu ya kodi ili kukuza uhiari wa ulipaji kodi. 

Akifungua semina hiyo Meneja wa TRA Mkoa wa Kagera, Bw. Castro John amewasisitiza washiriki kutunza kumbukumbu za biashara zao na kulitumia Dawati la uwezeshaji biashara kutatua changamoto na kupata ushauri wa biashara zao.

Hakuna maoni: