Breaking


Jumatano, 8 Oktoba 2025

NYAMAGANA TUPO TAYARI KUMLAKI RAIS SAMIA


UWANJA wa Nyamagana umefurika umati wa watu wakimsubiri kwa shauku kubwa mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama Cha Mapinduzi(CCM),Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan,ambaye Octoba 8,2025, anatarajiwa kuendelea na kampeni za kuomba ridhaa ya watanzania kushika dola.

Mkoa huo ni wa 22 ambapo jana baada ya kuwasili alifanya mkutano Buhongwa,Misungwi na Sengerema.

Akiwa katika mikoa hiyo ameahidi kuboresha huduma za maendeleo ya jamii na kuhakikisha zinafika karibu na wananchi.

Ameahidi ujenzi wa masoko,boti za uvuvi,zahanati,vituo vya afya na miundombinu ya barabara.

Msisitizo mkubwa anaotoa kwa wananchi ni kujitokeza kwenda kupiga kura Octoba 29,2025.

Hakuna maoni: