Breaking


Jumapili, 12 Oktoba 2025

RAIS SAMIA NI MTU KAZI MPENI KAZI

MGOMBEA ubunge wa Viti Maalum kupitia kundi la vijana kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi(CCM),Jesca Magufuli,amewaomba watanzania kumpa kura za ndio mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama hicho Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan,ili akaendeleze kazi kubwa na nzuri aliyoianza.

Amesema Rais Samia ni mtu wa kazi na katika kipindi chake amekamilisha miradi yote iliyoanzishwa na mtangulizi wake na kuanzisha mingine.

Jesca ambaye ni mtoto wa Rais wa awamu ya tano Hayati John Magufuli, amesema hayo Octoba 12,2025,wakati akizungumza katika mkutano wa kampeni wa mgombea Urais Dkt.Samia uliofanyika Wilaya ya Bukombe Mkoani Geita.

"Samia ni mtu wa kazi hivyo mpeni kazi akafanye kazi,wapeni kura wagombea ubunge pia na madiwani wa CCM,"amesema.

Ameeleza namna ilani ilivyowagusa vijana kupitia baadhi ya ahadi ikiwemo  kuzalisha ajira milioni 8,ujenzi wa vyuo vya ufundi stadi(VETA),na utoaji wa mikopo.

Hakuna maoni: