Mchezaji wa Sporting Morten Hjulmand, 26, ameibuka kama shabaha kuu ya Manchester United kuimarisha safu yao ya kiungo na klabu hiyo ya Ligi ya Premia ina matumaini ya kumpata Mdenmark huyo kwa takriban £50m. (Teamtalk)
Wamiliki wa Fulham wamemwambia kocha mkuu Marco Silva kuhusu nia yao ya kutaka kuongeza mkataba wake, ambao una kipengele cha kuachiliwa kwa pauni milioni 15. (The Athletic)
Barcelona na Real Madrid wanamfuatilia kwa karibu beki wa kati wa England Marc Guehi, 25, ambaye hataongeza mkataba wake na Crystal Palace baada ya mwisho wa msimu huu. (Fichajes)
#ChanzoBbcswahili

Hakuna maoni:
Chapisha Maoni