Breaking

Ijumaa, 3 Oktoba 2025

TETESI ZA SOKA ULAYA IJUMAA: REAL MADRID YATILIA SHAKA DILI LA KUTAKA KUMNUNUA IBRAHIMA KONATE

 

Uongozi mkuu wa Real Madrid una shaka kuhusu kutafuta dili la kumnunua mlinzi wa Liverpool na Ufaransa Ibrahima Konate, 26, ambaye mkataba wake unamalizika Anfield msimu ujao. (Fichajes - In Spanish)

Liverpool wamempanga beki wa kati wa Crystal Palace na Ufaransa Maxence Lacroix, 25, kama mbadala wa mchezaji mwenzake wa klabu, mlinzi wa Uingereza Marc Guehi, 25. (Football Insider)

Manchester United wamemuongeza kiungo wa kati wa Brentford na Ukraine Yehor Yarmolyuk mwenye umri wa miaka 21 kwenye orodha ya wachezaji wanaolengwa na uhamisho. (Caughtoffside)

Mshambulizi asiyekubalika wa Manchester United Joshua Zirkzee bado ana nia ya kutaka kujiunga na Juventus na AC Milan, huku mchezaji huyo wa kimataifa wa Uholanzi, 24, pia akilengwa kwa mkopo Januari na klbau ya Como. (ESPN), nje


Manchester United wamekamilisha mpango wa kumsajili kiungo wa kati wa Colombia Cristian Orozco, 17, kutoka klabu ya Bogota Fortaleza. (Fabrizio Romano),


#ChanzoBbcswahili

Hakuna maoni: