Breaking

Alhamisi, 16 Oktoba 2025

WATAKIWA KUWEKA MIKAKATI YA PAMOJA ILI KUBORESHA HUDUMA ZA DAMU SALAMA

 ‎‎

‎Mganga Mkuu wa Serikali Dkt. Grace Magembe amesema kuwa ushirikiano kwenye utekelezaji wa majukumu kati ya Mpango wa Taifa wa Damu Salama, Mikoa na Halmashauri ni nguzo muhimu  katika kurahisisha utendaji kazi na hivyo kuongeza ufanisi kwenye upatikanaji  wa damu salama kwa wananchi.‎

‎Dkt. Magembe ameyasema hayo  Oktoba 15, 2025 alipotembelea na kuzungumza na watumishi wa Wizara ya Afya, Mpango wa Taifa wa Damu Salama Kanda ya Ziwa, Jijini Mwanza ambapo pia alikagua  maabara na chumba maalum kwa ajili ya wachangia damu.‎

‎"Ushirikiano wa Mpango wa Damu Salama, Waganga Wakuu wa Mikoa na Halmashauri kutapelekea kupanga mikakati thabiti ya kuimarisha huduma za damu salama ikiwemo kuongeza wigo wa wachangiaji na kutatua changamoto zinazojitokeza"‎

‎Katika hatua nyingine amesema kuwa Serikali ya awamu ya sita kupitia Wizara ya Afya, imeagiza mashine kubwa zaidi mbili aina ya Alinity s  zenye uwezo wa kutoa majibu 600, sawa na sampuli 15.

Hakuna maoni: