Breaking

Jumatano, 26 Novemba 2025

DEBORA MWENDA KUPEPERUSHA BENDERA YA TANZANIA KWENYE BOXING ON BOXING DAY

 

Bondia Debora Mwenda ameahidi kuiwakilisha Tanzania dhidi ya Mariam Dick kutoka Malawi katika pambano la “Boxing On Boxing Day” litakalofanyika Desemba 26, 2025 kwenye Ukumbi wa Warehouse Masaki, Dar es Salaam.


Akizungumza mapema leo jijini Dar es Salaam, Debora amesema kuwa licha ya kuwa ni mara yake ya kwanza kushiriki katika pambano la kimataifa, anaamini ataonesha kiwango cha juu na kuipa Tanzania ushindi wa kishindo.


Naye kocha wake, Dickson Tembo, amesema kuwa Debora inaendelea na mazoezi makali na maandalizi yake yako vizuri, hivyo Watanzania wajiandae kushuhudia ushindi mkubwa siku ya pambano.


Katika upande mwingine, bondia Hassan Mwakinyo pia ataipeperusha bendera ya Tanzania, huku Hamadi Furahisha akitarajiwa kupambana na Mmalawi Hanock Phiri, pamoja na mapambano mengine yatakayowakutanisha Ally Ngwando, Mussa Makuka, na kwa upande wa wanawake Debora Mwenda dhidi ya Mariam Dick.


Pambano hilo litafanyika Desemba 26, 2025, katika ukumbi wa Warehouse Masaki kwenye tamasha la Boxing On Boxing Day.


#Official-Isharoja✍🏾✍🏾

Hakuna maoni: