Breaking

Jumanne, 11 Novemba 2025

ISRAEL YAIKATAA VIKOSI VYA UTURUKI KUINGIA GAZA, WAZIRI GIDEON SAAR ATOA KAULI KALI

 

Waziri wa mambo ya nje wa Israel Gideon Saar amesema kuwa Israel haitakubali kuwepo kwa wanajeshi wa Uturuki huko Gaza.

Maneno ya Saar yalikuwa matamshi ya wazi zaidi yaliyotolewa na Israeli kuhusu suala hili.

Akizungumza wakati wa ziara yake nchini Hungary, Saar amesema kuwa "TĂĽrkiye, chini ya uongozi wa [Rais] ErdoÄźan, ina mtazamo wa chuki dhidi ya Israel."

"Kwa hiyo, hatutaruhusu vikosi vyao vya kijeshi kuingia Ukanda wa Gaza, na tumewaambia hivi marafiki zetu wa Marekani," Gideon Saar alisema.

Suala hili pia lilijitokeza wakati wa ziara za Makamu wa Rais wa Marekani JD Vance na Waziri wa Mambo ya Nje Marco Rubio wiki iliyopita.

Hakuna maoni: