Breaking

Jumapili, 16 Novemba 2025

MC PILIPILI AFARIKI DUNIA


 Msanii wa vichekesho na MC, Emmanuel Mathias maarufu kama MC Pilipili, amefariki dunia leo, Novemba 16, 2025. Baadhi ya marafiki zake wa karibu wamethibitisha habari hii kwa Madelemo News, ambapo mwili wake unahifadhiwa kwenye Hospitali ya Mkoa wa Dodoma kwa sasa. 


Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya rufaa ya Dodoma, Dk Ernest Ibenzi amethibitisha kifo cha Emmanuel Mathias (MC Pilipili) .
Dk Ibenzi amesema kuwa leo Jumapili saa 11 walipokea mwili wa MC Pilipili ambao ulipelekwa hospitalini hapo na wasamaria wema.
"Ni kweli kati ya saa 10.30 ama 11 tulipokea mwili wa MC
Pilipili ambao uliletwa hospitalini hapa na wasamaria wema, maelezo mengine mtafute ofisa habari," amesema Dk Ibenzi.
MC Pilipili ni maliwa wa Dodoma na asili vake ni Wilaya va Bahi ingawa makazi yake mara nyingi yamekuwa Dodoma hasa mtaa wa Swaswa/lpagala.

Madelemo news inaendelea kufuatilia na kupata taarifa zaidi kuhusu chanzo cha kifo chake.


Hakuna maoni: