Breaking

Alhamisi, 20 Novemba 2025

NI LIVERPOOL PEKEE INAYOWEZA KUMSAJILI GUEHI – CRYSTAL PALACE


Klabu ya Crystal Palace imeeleza kuwa kwa sasa ni Liverpool pekee ndiyo yenye nafasi kubwa ya kumsajili beki wao mahiri, Marc Guehi, kutokana na uwezo wa kifedha na mpango wa muda mrefu wa timu hiyo. Ripoti zinaeleza kuwa Palace haitarajii kumruhusu nyota huyo kuondoka kirahisi, lakini wapo tayari kusikiliza ofa itakayokidhi thamani waliyoiweka.


Liverpool imekuwa ikimfuatilia Guehi kwa muda mrefu kama sehemu ya kuimarisha safu yao ya ulinzi, hasa baada ya kuonekana wazi wanahitaji kuongeza nguvu mpya kwenye eneo hilo. Beki huyo wa England amekuwa mchezaji muhimu kwa Crystal Palace, na uhamisho wake unatarajiwa kuwa miongoni mwa dili kubwa katika dirisha lijalo.


Hakuna maoni: