Sehemu ya Tatu – Siri ya Neema
Wiki mbili zilipita tangu tukutane tena.
Kila jioni tulikuwa tukionana, tukizungumza kuhusu maisha, ndoto, na mambo madogo ambayo yalifanya dunia ionekane nyepesi.
Nilianza kuamini kuwa huenda Neema alikuwa mwanzo wa kitu kipya maishani mwangu kitu safi, halisi, na cha amani.
Lakini siku moja mambo yalibadilika.
Nilifika pale mahali petu pa kukutana, nikiwa nimebeba maua niliyomuahidi.
Nilikaa kwenye benchi lile, nikingoja dakika tano… kisha kumi… hadi dakika arobaini.ππππ
Neema hakutokea.
Nilipoamua kuondoka, nilimsikia mtu akinong’ona nyuma yangu,
“Unamtafuta Neema?”
Niligeuka haraka. Alikuwa ni mwanamke wa makamo, mwenye uso wa huzuni.
“Ndio,” nilijibu kwa haraka. “Umemuona?”
Alinitazama kwa muda, kisha akasema kwa sauti ya chini,
“Kijana… Neema aliyekuwa anakaa hapa, alifariki wiki mbili zilizopita.”
Nilihisi dunia ikigeuka kimya.
“Mmh… unasema nini?” nilishindwa kuamini.π³π³π³π³π³
“Mwanangu alikuwa akipenda kukaa hapa kila jioni, hasa alipokuwa anakumbuka mama yake. Alifariki ghafla usiku ule ule wa Jumamosi kabla ya mazishi ya mama yake,” alisema yule mama huku machozi yakimtoka.
Nilihisi miguu yangu ikitetemeka.πππππ
Nilijaribu kusema, lakini sauti ikakataa kutoka.
Lakini… nilikuwa nimemuona Neema wiki mbili zilizopita. Nilizungumza naye. Tulicheka. Tulishikana mikono.
Kwa muda huo wote nilikuwa nikiwasiliana na nani? π’π
Niliondoka pale nikiwa nimechanganyikiwa, nikikumbuka maneno yake:
“Wakati mwingine mwanga unaokuongoza hauji kutoka juu, bali kutoka kwa mtu anayekaa karibu yako kimya.”
Labda Neema alikuwa mwanga huo… aliyekuja kunionyesha njia, kisha akatoweka.
π‘ Somo la Sehemu ya Tatu:
Wapo watu wanaokuja kwenye maisha yetu kwa muda mfupi si kwa bahati, bali kwa kusudi. Wanatuacha, lakini nuru yao hubaki ikituongoza milele.
Haya Ndugu zangu Neema ndio hivyo kama mlivyosikiaπππ
π―️ Endelea kufuatilia Sehemu ya Nne hapa KONA YA SIMULIZI ndani ya Madelemo News.

Hakuna maoni:
Chapisha Maoni