Breaking


Alhamisi, 6 Novemba 2025

TETESI ZA SOKA ULAYA ALHAMISI: REAL MADRID YAJIONDOA KWENYE MBIO ZA KUMSAJILI GUEHI

 

Real Madrid imejiondoa kwenye kinyang'anyiro cha kumsajili Mchezaji wa Crystal Palace Marc Guehi, 25, ambaye kandarasi yake inamalizika msimu huu wa joto kwa sababu ya mshahara mkubwa na mahitaji mengine, huku Liverpool na Bayern Munich wakipigiwa upatu kumnunua mlinzi huyo wa Uingereza. (AS - kwa Kihispania)

Vilabu kadhaa vya Ligi ya Premia vina nia ya kumsajili beki wa Feyenoord Mholanzi Givairo Read mwenye umri wa miaka 19 lakini wanakabiliwa na ushindani kutoka kwa Bayern Munich. (Teamtalk)

Tottenham na Liverpool zinamnyatia beki wa Ugiriki anayekipiga Wolfsburg Ujerumani Konstantinos Koulieraki, 21. (TBR Football)

#ChanzoBbcswahili

Hakuna maoni: