Breaking

Jumamosi, 22 Novemba 2025

UTABIRI WA HALI YA HEWA KWA SAA 24 ZIJAZO

 

Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania imetoa utabiri wa saa 24 zijazo kuanzia saa 3 usiku wa leo, tarehe 22 Novemba 2025.


Mikoa ya Tabora, Katavi, Kigoma, Kagera, Geita, Mwanza, Ruvuma, Rukwa, Iringa, Njombe, Songwe na Mbeya inatarajiwa kuwa na mawingu kiasi, mvua na ngurumo katika maeneo machache pamoja na vipindi vya jua.


Mikoa ya Lindi, Mtwara, Manyara, Arusha, Kilimanjaro, Morogoro, Dar es Salaam na Tanga, pamoja na Pwani ikijumuisha Visiwa vya Mafia, pamoja na Unguja na Pemba, inatarajiwa kuwa na mvua nyepesi katika maeneo machache na vipindi vya jua.


Mikoa ya Singida, Dodoma, Shinyanga, Simiyu na Mara inatarajiwa kuwa na mawingu kiasi na vipindi vya jua.


Kwa upande wa hali ya pwani, upepo unatarajiwa kuvuma kutoka kaskazini mashariki kwa kasi ya kilomita 20 kwa saa, na bahari ikiwa na mawimbi madogo.


Mabadiliko madogo yanatarajiwa siku ya Jumatatu, tarehe 24 Novemba 2025.


Utabiri umetolewa na Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania.


Hakuna maoni: