Vumbi la usajili Ulaya limeanza kuvuka mipaka, na jina la kijana hatari Myles Lewis-Skelly linatajwa kila kona!
Kiungo huyo chipukizi wa Arsenal ameweka vilabu vikubwa kwenye taharuki, huku Manchester United, Chelsea, Bayern Munich na AC Milan zikiripotiwa kumtupia macho kwa ukaribu.
Lewis-Skelly, anayejulikana kwa kasi, nidhamu na uwezo wa kupiga pasi za hatari katikati ya uwanja, amekuwa kivutio kikubwa baada ya kung’ara kwenye mechi za vijana wa Arsenal.
Kwa mujibu wa duru za ndani, vilabu hivyo vinapanga kutoa dau nono Januari ili kumvuta kabla ya msimu ujao.
Mashabiki wengi wanaamini kijana huyu ndiye “gemu-changer” wa kizazi kipya – na dirisha dogo la usajili linaonekana litawaka moto zaidi ya kawaida! 🔥

Hakuna maoni:
Chapisha Maoni