Watu 44 wamefariki na wengine zaidi ya 270 haijulikani walipo huko Hong Kong, kufuatia ajali mbaya ya moto iliyotokea kwenye majengo kadhaa ya ghorofa.
Wakati zoezi la uokoaji likiendelea, mamlaka za Hong Kong zimesema kwa sasa moto huo umedhibitiwa na kwamba uchunguzi umeanzishwa, huku watu watatu wakikamatwa kwa tuhuma za mauaji bila kukusudia kuhusiana na moto huo uliozuka katika kitongoji kipya cha makazi wilayani Tai Po.
Mamlaka za Hong Kong zimesema zinachunguza ikiwa kulikuwa na vifaa hatari nje ya majengo na ikiwa ujenzi ulikidhi viwango vya kuhimili moto, kwani kulishuhudiwa hali isiyo ya kawaida ya kuenea kwa kasi kwa moto huo.

Hakuna maoni:
Chapisha Maoni