Breaking


Jumatano, 24 Desemba 2025

BANK YA AMANA KUENDELEA KUSHIRIKIANA NA TRA

Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Bw. Yusuph Juma Mwenda, leo tarehe 24.12.2025 amekutana na kufanya mazungumzo na Mkurugenzi Mtendaji wa Bank ya Amana, Bw. Abubakar Athman Ali, katika ofisi za TRA jijini Dar es Salaam kwa lengo la kuimarisha ushirikiano kati ya taasisi hizo mbili.

Katika kikao hicho, viongozi hao wamejadili maeneo mbalimbali ya ushirikiano ikiwemo kuboresha mifumo ya ulipaji kodi kupitia taasisi za kifedha, pamoja na kuhamasisha walipakodi kulipa kodi kwa hiari kwa kutumia huduma za kibenki.

Bw. Abubakar amesema Bank ya Amana ipo tayari kushirikiana kwa karibu na TRA katika kuhakikisha huduma bora zinapatikana kwa walipakodi, huku akiweka mkazo kwenye uboreshaji wa mifumo na elimu ya kodi kwa wateja wa benki hiyo.

Kwa upande wake, Kamishna Mkuu Bw. Mwenda amepongeza ushirikiano huo na kusema kuwa hatua kama hizo zinaimarisha mazingira ya ulipaji kodi na kuchangia katika kukuza mapato ya Taifa.

Hakuna maoni: