Tume ya Madini imetoa bei elekezi za madini kwa tarehe 2 Desemba 2025.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo, bei ya kimataifa ya dhahabu imefikia dola za Marekani 4,275.53 kwa toz, huku bei ya soko la dunia ikikadiriwa kuwa shilingi 336,619.55 kwa gramu.
Aidha, bei ya soko la madini hapa nchini kwa gramu moja ya dhahabu imeainishwa kuwa shilingi 302,957.59, na katika vituo vya ununuzi, dhahabu inanunuliwa kwa shilingi 296,225.20 kwa gramu.
Hizo ndizo bei elekezi za madini zilizotolewa na Tume ya Madini kwa siku ya leo.


Hakuna maoni:
Chapisha Maoni