Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Ashatu Kijaji, amehitimisha ziara yake Mkoani Iringa kwa kukagua maendeleo ya ujenzi wa Jengo la Kituo cha Utalii pamoja na Jengo la Ofisi Mpya za Taasisi ya Utafiti wa Wanyamapori Tanzania (TAWIRI), yaliyopo Kihesakilolo, Manispaa ya Iringa.
Katika ziara hiyo, Waziri Kijaji aliambatana na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Hamad Chande, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Bw. Nkoba Mabula, pamoja na viongozi wengine wa Wizara.
Ukaguzi huo ulikuwa na lengo la kutathmini maendeleo ya miradi hiyo muhimu inayotarajiwa kuimarisha shughuli za utalii na tafiti za wanyamapori nchini, hususan katika Ukanda wa Nyanda za Juu Kusini.




Hakuna maoni:
Chapisha Maoni