Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Hali ya hewa Tanzania (TMA) na Mwakilishi wa kudumu wa Tanzania katika Shirika la Hali ya Hewa Duniani(WMO), Dkt. Ladislaus Chang'a alifungua mafunzo ya usimamizi wa miradi ya maendeleo kwa menejimenti ya Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) yanayoendeshwa na Chuo Cha Uhasibu Arusha (IAA), ambapo mafunzo hayo yamejikita zaidi katika usimamizi wa miradi ya uwekezaji wa miundombinu kama “Capital Expenditure (CapEx)”.
Dkt. Chang'a katika ufunguzi alisema kuwa TMA ikiwa ni Taasisi ya Serikali iliyopewa majukumu ya kutoa huduma za hali ya hewa, kuratibu na kudhibiti shughuli zote zinazohusiana na masuala ya hali ya hewa nchini. Mamlaka inashiriki pia kutekeleza miradi mbalimbali yenye malengo yanayochangia kufanikisha utekelezaji wa majukumu ya TMA ya kitaifa, kikanda na kimataifa.
Aidha, alieleza kuwa miongoni mwa miradi ambayo inatekelezwa na TMA ni ikiwemo miradi ya uwekezaji wa miundombinu mbalimbali “Capital Expenditure (CapEx)”, Ujenzi wa Kituo cha Ufuatiliaji wa matukio ya Tsunami (Tsunami Centre), TMA inapata ufadhili wa kujenga vituo vipya vitatu (3) vya kupima hali ya hewa katika anga za juu kupitia mradi wa (SOFF) na nyinginezo nyingi.
Kwa upande wake Mtiva wa Kitivo cha Mafunzo ya Insia na Sayansi za Jamii, Dkt. Leticia Rwabishungi wa chuo Cha Uhasibu Arusha aliwashukuru sana TMA kwa kufika IAA kwa mafunzo ya usimamizi wa miradi na kusema chuo kina kozi nyingi sio tu Uhasibu bali kozi mbalimbali na kwa ngazi zote hivyo aliwakaribisha kuendelea kupata mafunzo katika chuo cha IAA.
Mojawapo ya walioshiriki katika ufunguzi wa mafunzo hayo ni Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania, Mkurugenzi wa Huduma za Ushauri wa Chuo cha IAA, Menejimenti ya Mamlaka ya Hali ya Hewa, Wakufunzi kutoka Chuo cha IAA, Wataalamu mbalimbali kutoka TMA, IAA na UNDP.
Mafunzo haya yameanza Disemba 15 mpka 19, mwaka 2025.





Hakuna maoni:
Chapisha Maoni