Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi moja ya vipaumbele vyake ni katika mwaka wa fedha 2025/2026 ni kuongeza kasi ya upangaji, upimaji, umilikishaji na usajili wa ardhi mijini, vijijini na katika maeneo ya kimkakati.
Malima amesema hayo Desemba12, 2025 alipokutana na Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dokta Leonard Akwilapo aliyekuwa mkoani humo kwa ajili ya kuhudhuria mahafali ya 44 ya Chuo cha Ardhi Morogoro .
Amesema, migogoro ya ardhi katika mkoa wake wa Morogoro imepungua kwa kiasi kikubwa kutokana na juhudi kubwa za wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi kupitia ofisi ya Kamishna wa Ardhi Msaidizi mkoa ambapo imefanya kazi kubwa ya kufikia wananchi kupitia Kliniki ya Ardhi.
Kwa upande wake Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dokta Akwilapo amemueleza mkuu wa mkoa wa Morogoro kuwa, wizara yake kwa sasa inafanya juhudi kubwa kuhakikisha migogoro ya ardhi iliyopo inatatuliwa na hakuna migogoro mipya inayozalishwa kwenye maeneo mbalimbali nchini.
Aidha, Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi amezihimiza taasisi za umma kuhakikisha zinalinda maeneo yao ili kuepuka uvamizi alioueleza kuwa ndiyo unaochangia kwa kikubwa migogoro ya ardhi katika maeneo ya umma.


Hakuna maoni:
Chapisha Maoni