Tume ya Madini nchini Tanzania imeendelea kutekeleza jukumu lake la kusimamia na kuratibu shughuli za madini kwa kuweka wazi taarifa muhimu za soko, ikiwemo bei elekezi za madini. Hatua hii inalenga kuwasaidia wachimbaji wadogo, wafanyabiashara na wadau wengine wa sekta ya madini kupata taarifa sahihi na za wakati kuhusu mwenendo wa bei katika soko la dunia na la ndani.
Kwa mujibu wa bei elekezi za madini zilizotolewa tarehe 15 Desemba 2025, bei za dhahabu na fedha zimeonesha mabadiliko kulingana na soko la dunia na soko la madini nchini, kama ifuatavyo:
BEI ELEKEZI ZA DHAHABU (GOLD)
- Bei ya Soko la Dunia:
USD 4,361.95 kwa aunzi (toz) - Bei ya Soko la Dunia kwa Tanzania:
TZS 344,033.58 kwa gramu - Bei ya Soko la Madini (Mineral Market Price):
TZS 309,630.22 kwa gramu - Bei ya Kituo cha Ununuzi (Buying Centre Price):
TZS 302,749.55 kwa gramu
BEI ELEKEZI ZA FEDHA (SILVER)
- Bei ya Soko la Dunia:
USD 64.51 kwa aunzi (toz) - Bei ya Soko la Dunia kwa Tanzania:
TZS 5,088.00 kwa gramu - Bei ya Soko la Madini (Mineral Market Price):
TZS 4,579.20 kwa gramu - Bei ya Kituo cha Ununuzi (Buying Centre Price):
TZS 4,477.44 kwa gramu
Tume ya Madini imeendelea kuhimiza wadau wa sekta ya madini kufuatilia bei hizi elekezi mara kwa mara ili kufanya maamuzi sahihi ya kibiashara na kuhakikisha wanazingatia taratibu na miongozo iliyowekwa na Serikali.


Hakuna maoni:
Chapisha Maoni