Breaking


Jumapili, 28 Desemba 2025

NMB YADHAMINI MAPINDUZI CUP 2026

 Katika kuendeleza dhamira ya kuyaenzi Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar, Benki ya NMB imesaini Hati ya Makubaliano (MoU) na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) kwa ajili ya kudhamini mashindano ya NMB Mapinduzi Cup 2026, ambapo benki hiyo itakuwa Mdhamini Mkuu wa mashindano hayo.


Ushirikiano huu unaonesha kwa vitendo dhamira ya Benki ya NMB kushirikiana kwa karibu na Serikali katika kukuza na kuendeleza michezo kama chombo muhimu cha kuimarisha mshikamano wa kitaifa, kuibua na kukuza vipaji vya vijana pamoja na kuitangaza Zanzibar katika anga la kimataifa.




Kupitia udhamini huu, NMB inalenga si tu kufanikisha mashindano ya Mapinduzi Cup, bali pia kuchangia juhudi za kuitangaza Zanzibar kama kitovu cha michezo, utalii na fursa mbalimbali za uwekezaji. Hatua hii ni sehemu ya mchango wa sekta binafsi katika kuunga mkono maendeleo ya kijamii na kiuchumi ya Zanzibar na Tanzania kwa ujumla.


#NMBKaribuYako


Hakuna maoni: