Breaking


Jumatano, 31 Desemba 2025

RAIS DKT MWINYI AUNDA TUME YA KUPITIA NA KUTATHMINI MASUALA YA FIDIA






Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi, ameunda rasmi Tume Maalum ya Kupitia na Kutathmini Masuala ya Fidia yanayotokana na utekelezaji wa miradi mbalimbali ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) katika maeneo ya Unguja na Pemba.


Kuundwa kwa tume hiyo kunalenga kushughulikia kwa kina changamoto za fidia zilizojitokeza wakati wa utekelezaji wa miradi ya maendeleo, ikiwemo malalamiko ya wananchi na taasisi zilizoathiriwa. Kupitia tume hii, Serikali inalenga kupata mapendekezo ya kitaalamu yatakayosaidia kuboresha mifumo ya fidia na kuhakikisha haki, uwazi na ufanisi vinazingatiwa.


Tume hiyo ina jukumu la kupitia kwa kina masuala yote ya fidia, kubaini changamoto zilizopo, pamoja na kuishauri Serikali juu ya hatua stahiki za kuchukua ili kulinda maslahi ya wananchi na kuimarisha utekelezaji wa miradi ya maendeleo kwa mustakabali wa Zanzibar.


Hakuna maoni: