Mamlaka ya hali ya hewa imetoa utabiri wa hali ya hewa kwa kipindi cha saa 24 zijazo kuanzia saa 3.00 usiku wa leo, tarehe 26 Desemba 2025, ikionya kuwepo kwa mvua, mawingu na ngurumo katika maeneo mbalimbali nchini.
ANGALIZO MUHIMU
Vipindi vifupi vya mvua kubwa vinatarajiwa katika baadhi ya maeneo ya mikoa ya Arusha, Kilimanjaro, Manyara, Singida, Dodoma, Morogoro, Lindi na Mtwara. Wananchi wanashauriwa kuchukua tahadhari, hasa maeneo yenye miinuko, mabonde na yanayokumbwa na mafuriko mara kwa mara.

Hakuna maoni:
Chapisha Maoni