Utabiri wa hali ya hewa kwa saa 24 zijazo, kuanzia saa tatu usiku wa leo, tarehe tatu Disemba mwaka 2025.
Kwa mikoa ya Kagera na Kigoma, kutakuwa na mawingu kiasi, mvua na ngurumo katika maeneo machache pamoja na vipindi vya jua.
Visiwa vya Unguja na Pemba, pamoja na mikoa ya Dar es Salaam, Tanga na Pwani ikijumuisha Mafia, vinatarajiwa kuwa na mawingu kiasi, mvua nyepesi katika maeneo machache na vipindi vya jua.
Mikoa ya Mtwara, Lindi, Katavi, Tabora, Morogoro, Singida, Dodoma, Arusha, Manyara, Kilimanjaro, pamoja na Kanda ya Ziwa inayojumuisha Geita, Mwanza, Shinyanga, Simiyu na Mara; sambamba na mikoa ya Ruvuma, Rukwa, Iringa, Njombe, Songwe na Mbeya, inatarajiwa kuwa na hali ya mawingu kiasi na vipindi vya jua.
Upepo wa Pwani unatarajiwa kuvuma kutoka Kaskazini Mashariki kwa kasi ya kilomita 20 kwa saa, huku bahari ikitarajiwa kuwa na mawimbi madogo.
Matarajio kwa siku ya Ijumaa tarehe tano Disemba ni mabadiliko madogo ya hali ya hewa.
Utabiri huu umetolewa na Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania, TMA, tarehe tatu Disemba, mwaka 2025.

Hakuna maoni:
Chapisha Maoni