HOSPITALI ya Benjamin Mkapa ikishirikiana na Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Singida,imeweka kambi mkoani humo kutoa huduma za uchunguzi na matibabu ya moyo kwa watoto na watu wazima.
Akieleza kuhusiana na kambi hiyo Kaimu Mkurugenzi msaidizi wa mafunzo na huduma mkoba na Mkuu Rayhan Mbisso amesema hiyo ni fursa kwa wananchi wa Singida kuweza kufanya uchunguzi na kupata matibabu kupitia madaktari bingwa walioambatana nao.
"Tumekuja na madaktari bingwa wa moyo kwa watu wazima na watoto, hii inatoa fursa kubwa kwa Wananchi wa mkoa wa singida kufanya uchunguzi na kupata matibabu ya Moyo kwa watoto kwa siku tano mfululizo kuanzia leo"amesema Mbisso
Kaimu Mganga mfawidhi Dkt. David Mwasota amewapokea madaktari Bingwa na Wataalamu wa matibabu ya moyo kutoka Hospitali ya Benjamin Mkapa na kueleza kiu ya wananchi wa Mkoa huo.
"Tumetangaza ujio wenu na mwitikio wa siku ya kwanza ni mkubwa wanawasubiri muweze kuwapa huduma, nimatumaini yetu siku zinavyo endelea tutakuwa na wagonjwa wengi zaidi ya siku ya leo"amesema Dkt. Mwasota
Hospitali ya Benjamin Mkapa imetoa madaktari na wataalamu wa mayo ikiwa ni sehemu ya kuimarisha huduma katika maeneo yanayo izunguka Hospitali hiyo na huku ikiendelea kuadhimisha miaka kumi ya utoaji huduma zake tangia ilipo anzishwa.




Hakuna maoni:
Chapisha Maoni