Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Ashatu Kijaji (Mb) ameupongeza uongozi wa Chuo cha Taifa cha Utalii Tanzania (NCT) kwa kazi nzuri inayofanya ya kumtoa elimu bora ya fani mbalimbali ya Utalii hususani ukarimu hali inayo ongeza ubora katika utoaji huduma kwa wageni mbalimbali wanaotembelea vivutio vya kitalii nchini.
Dkt. Kijaji amezitoa pongezi hizo Jijini Dar es Salaam kwe Mahafali ya 23 ya chuo hicho katika fani mbalimbali ya sekta ya Utalii.
Aidha Dkt. Kijaji amewataka wahitimu hao, kuwa mfano katika utoaji wa huduma bora kwa wageni kama sehemu ya kurejesha shukrani kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kazi kubwa na nzuri ya kuifungua sekta ya Utalii nchini ambayo inaendelea kukua kila mwaka tangu alipoingia madarakani mwaka.
Katika maonesho hayo yaliyoudhuriwa na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Dkt. Hassan Abbasi, Wakuru wa Idara, Vitengo na Taasisi za wa Wizara hiyo, pamoja na wageni mbalimbali, wahitimu hao walionesha umahiri mkubwa katika fani mbalimbali hususani ya Ukarimu na maandalizi ya vyakula mbalimbali vya kuvutia.





Hakuna maoni:
Chapisha Maoni