Breaking


Jumamosi, 10 Januari 2026

DKT TULIA AKABIDHI VIFAA NA SARE ZA SHULE KWA WANAFUNZI 3,000

Katika kuunga mkono juhudi za kuinua kiwango cha elimu mkoani Mbeya, Mbunge wa Mbeya Dkt. Tulia Akson,  leo  amekabidhi sare za shule na vifaa mbalimbali vya shule kwa wanafunzi 3,000 kutoka kata mbalimbali za jiji hilo.

Akizungumza katika hafla ya ugawaji iliyofanyika katika viwanja vya shule ya msingi Hasanga ,Mbunge huyo alisema kuwa lengo kuu ni kuhakikisha kila mtoto anapata fursa ya kusoma bila vikwazo vya ukosefu wa sare au vifaa vya msingi.

“Watoto hawa ndio taifa la kesho, tusipowekeza kwao leo, tutajuta baadaye. Hii ni sehemu ya dhamira yangu ya kuhakikisha elimu inakuwa jumuishi na inayofikika kwa wote,” alisema Mbunge huyo.

Aidha, aliahidi kuwa zoezi hilo litakuwa endelevu  zaidi, hasa kwenye kaya zenye changamoto.

Wazazi waliokuwepo waliishukuru ofisi ya Mbunge kwa moyo huo wa kutoa, wakisema msaada huo umepunguza mzigo mkubwa kwa familia nyingi zenye hali duni.

Hakuna maoni: