Breaking


Jumanne, 13 Januari 2026

𝗗𝗞𝗧. 𝗠𝗜𝗚𝗜𝗥𝗢 𝗔𝗪𝗔𝗦𝗜𝗟𝗜 𝗜𝗟𝗔𝗟𝗔 KUIMARISHA 𝗨𝗛𝗔𝗜 𝗪𝗔 𝗖𝗖𝗠 𝗠𝗔𝗦𝗛𝗜𝗡𝗔𝗡𝗜

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dkt. Asha-Rose Migiro, amewasili katika Ukumbi wa Diamond Jubilee, Wilaya ya Ilala, kwa ajili ya ziara iliyoambatana na kikao kazi na Mabalozi wa Mashina wa Wilaya hiyo, ikiwa na lengo la kuimarisha uhai wa Chama kuanzia ngazi za chini.

Katika ziara hiyo, Dkt. Migiro ameambatana na viongozi mbalimbali wa Chama, akiwemo Katibu wa NEC Itikadi, Uenezi na Mafunzo, Kenani Kihongosi.

Ziara hiyo inahitimisha mfululizo wa ziara ya Katibu Mkuu katika Mkoa wa Dar es Salaam, baada ya kutembelea Wilaya za Temeke, Kigamboni, Kinondoni na Ubungo, kabla ya kuhitimisha leo katika Wilaya ya Ilala.

Hakuna maoni: