Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi, amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Japan nchini Tanzania, Mhe. Mikami Yoichi, katika Ikulu ya Chamwino mkoani Dodoma, leo tarehe 14 Januari 2025.
Mazungumzo hayo yalilenga kuimarisha na kukuza zaidi ushirikiano wa kidiplomasia na maendeleo kati ya Tanzania na Japan, hususan katika maeneo ya kimkakati yanayochangia ustawi wa pande zote mbili. Viongozi hao walisisitiza dhamira ya kuendeleza uhusiano wa kihistoria uliopo, kwa maslahi mapana ya wananchi wa mataifa hayo mawili.






Hakuna maoni:
Chapisha Maoni