Karibu kwenye Meza ya Magazeti ya leo, Jumamosi Januari 03, 2026, ambapo kurasa za mbele za magazeti zimejaa taarifa nzito zinazogusa uchumi, siasa, ajali, miundombinu na michezo.
Gazeti la Mwananchi limeandika kwa uzito kuhusu uharibifu wa reli ya kisasa ya SGR unaoibua maswali mengi, huku pia likiripoti ajali ya Morogoro iliyotambuliwa kwa njia ya DNA, pamoja na sakata la uteuzi wa Chadema Nyasa na kesi ya kitendo cha kikatili cha mmarekani aliyedakwa na mabomu.
Upande wa michezo, MwanaSpoti limejikita katika msisimko wa AFCON, likitangaza huko Morocco, Acha Kipigwe Tu, huku macho yote yakielekezwa kwenye mechi muhimu za leo na mustakabali wa nyota mbalimbali. Aidha, limeandika kuhusu mrithi wa Ahouna kuyu hapa, mustakabali wa wachezaji, pamoja na taarifa moto za ligi na soka la kimataifa.
Kwa ujumla, Meza ya Magazeti ya leo inakuletea taswira pana ya matukio yanayoitikisa nchi na dunia, kuanzia hoja nzito za kitaifa hadi burudani na ushindani wa michezo usikose muhtasari huu wa kina.














Hakuna maoni:
Chapisha Maoni