Waziri wa Fedha, Mhe. Balozi Khamis Mussa Omar (Mb), amekutana na kufanya mazungumzo na Katibu wa Chama cha Mapinduzi CCM mkoa wa Arusha, Bw. Mussa Dadi Matoroka na kutumia fursa hiyo kuwaasa watanzania wote kudumisha upendo, amani na mshikamano ili nchi iweze kuwa tulivu na kupiga hatua kubwa za maendeleo.
Kwa upande wake, Katibu wa CCM mkoa wa Arusha, Bw. Mussa Dadi Matoroka, alisisitiza kuwa amani, upendo na mshikamano ni nguzo kuu ya maendeleo na kwamba chama chake kitaendelea kuhubiri amani miongoni mwa watanzania ili nchi iwe na maendeleo katika nyanja zote za kiuchumi na kijamii.
Alisema kuwa mkoa wa Arusha hivi sasa uko shwari na wananchi Wanaendelea na kazi zao za kuwapatia kipato katika sekta za biashara, utalii na nyingine nyingi.
Kikao hicho kilihudhuriwa pia na Naibu Waziri wa Fedha, Mhe. Laurent Luswetula (Mb), pamoja na maafisa wengine waandamizi wa Chama hicho.






Hakuna maoni:
Chapisha Maoni