Naibu Waziri wa Mambo ya Nje anayeshughulikia masuala ya Afrika Mashariki Mhe. James Kinyasi Millya (Mb.) ametembelea Kituo cha Utoaji Huduma kwa Pamoja Mpakani ( _One Stop Boarder Post-OSBP_ ) cha Namanga kilichopo mkoani Arusha Januari 24,2026.
Akitembelea kituoni hapo, Mhe Millya alipokelewa na Meneja wa Mamlaka ya Mapato mkoa wa Arusha Bw. Deogratius Shuma na wawakilishi kutoka Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Longido na watumishi wa taasisi 18 za Serikali zinazotoa huduma katima kituo hicho.
Mhe Waziri Milya pia alikutana na viongozi wa Jumuiya ya Wafanyabiashara mpakani ikiwemo TAFFA, CHAWAMATA, TCCIA, na Wanawake Wajasiliamali Mpakani.
Akizungumza na wadau kituoni hapo Mhe. Millya amesema mpaka wa Namanga ni moja kati ya vituo vikubwa na kitovu cha kiuchumi kati ya Tanzania na Kenya kutokana na usafirishaji wa bidhaa za viwandani, mazao ya kilimo, huduma za utalii na muingiliano wa wananchi ki fursa kati ya nchi mbili.








Hakuna maoni:
Chapisha Maoni