Tume ya Madini imetangaza rasmi bei elekezi za madini kwa tarehe 09 Januari, 2026, zikihusisha madini ya Dhahabu (Gold) na Fedha (Silver). Bei hizo hutumika kama mwongozo wa biashara ya madini kwa wachimbaji, wafanyabiashara pamoja na vituo vya ununuzi nchini.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo, bei elekezi za Dhahabu katika soko la dunia zimefikia USD 4,477.70 kwa wakia (toz) sawa na TZS 355,647.73 kwa gramu, huku bei ya soko la madini nchini ikiwa TZS 320,082.96 kwa gramu.
Aidha, kwa upande wa Fedha, bei ya soko la dunia imefikia USD 76.51 kwa wakia (toz) sawa na TZS 6,076.92 kwa gramu. Bei ya soko la madini nchini imewekwa kuwa TZS 5,469.22 kwa gramu, huku bei elekezi ya vituo vya ununuzi ikiwa TZS 5,347.69 kwa gramu.
Tume ya Madini imeeleza kuwa bei hizo zinalenga kuhakikisha uwazi, haki na uthabiti wa biashara ya madini, sambamba na kulinda maslahi ya wachimbaji na wawekezaji katika sekta ya madini nchini.
Wananchi na wadau wa sekta ya madini wanahimizwa kuzingatia bei hizo katika shughuli zao za kila siku.


Hakuna maoni:
Chapisha Maoni