Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kupitia Rais wake Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, imeizawadia Timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) shilingi milioni 500 kufuatia kufanikiwa kufuzu hadi hatua ya 16 bora katika michuano ya Mataifa ya Afrika (AFCON).
Taarifa hiyo imetolewa na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Mwigulu Nchemba, wakati akizungumza na wachezaji pamoja na benchi la ufundi la Taifa Stars kwa njia ya simu. Mazungumzo hayo yalifanyika wakati timu hiyo ilipotembelewa na Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Paul Makonda.
Akizungumza, Waziri Mkuu Nchemba amesema Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan amewapongeza wachezaji, benchi la ufundi pamoja na Watanzania wote kwa mafanikio hayo ya kihistoria, na kusisitiza kuwa serikali itaendelea kuwaunga mkono.
Aidha, Waziri Mkuu ameongeza kuwa Rais Samia ameahidi kutoa zawadi nono zaidi endapo Taifa Stars itaendelea kufanya vizuri na kufanikiwa kutinga hatua ya robo fainali ya michuano hiyo inayoendelea nchini Morocco.




Hakuna maoni:
Chapisha Maoni