Breaking


Jumapili, 4 Januari 2026

TABIRI WA HALI YA HEWA KWA SAA 24 ZIJAZO




Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imetoa utabiri wa hali ya hewa kwa saa 24 zijazo kwa maeneo mbalimbali ya nchi kama ifuatavyo:


🌧️ Mvua na Ngurumo kwa Vipindi

Mikoa ya Morogoro, Lindi na Mtwara

Inatarajiwa hali ya mawingu, mvua na ngurumo katika maeneo machache kwa vipindi vifupi vya jua.


Mikoa ya Rukwa, Songwe, Mbeya, Iringa, Njombe na Ruvuma

Hali ya mawingu kiasi, mvua na ngurumo katika maeneo machache pamoja na vipindi vya jua.


Mkoa wa Manyara

Mawingu kiasi yakifuatana na mvua na ngurumo katika maeneo machache.


Mikoa ya Dodoma na Singida

Inatarajiwa mawingu kiasi pamoja na mvua za hapa na pale na vipindi vya jua.


Mikoa ya Kigoma, Tabora na Katavi

Hali ya mawingu kiasi, mvua na ngurumo katika baadhi ya maeneo.


Mikoa ya Kagera, Geita, Mwanza, Shinyanga, Mara na Simiyu

Mawingu kiasi, mvua na ngurumo katika maeneo machache pamoja na vipindi vya jua.



🌦️ Mvua Nyepesi na Vipindi vya Jua

Visiwa vya Unguja na Pemba

Hali ya mawingu kiasi, mvua nyepesi katika maeneo machache na vipindi vya jua.


Mikoa ya Arusha na Kilimanjaro

Mawingu kiasi, mvua nyepesi katika maeneo machache na vipindi vya jua.


Mikoa ya Tanga na Dar es Salaam

Inatarajiwa hali ya mawingu kiasi, mvua nyepesi na vipindi vya jua.


Mkoa wa Pwani (ikijumuisha Visiwa vya Mafia)

Hali ya mawingu kiasi, mvua nyepesi katika baadhi ya maeneo na vipindi vya jua.





⚠️ ANGALIZO LA HALI HATARISHI

Vipindi vifupi vya upepo mkali unaofikia kilomita 40 kwa saa pamoja na mawimbi makubwa yanayofikia mita 2 vinatarajiwa katika baadhi ya maeneo ya ukanda wa pwani ya Bahari ya Hindi.


Maeneo yanayoweza kuathirika ni:


  • Tanga
  • Dar es Salaam
  • Pwani (ikiwemo Mafia)
  • Lindi
  • Mtwara
  • Visiwa vya Unguja na Pemba

Wananchi hususan wavuvi, wasafiri wa majini na wakazi wa maeneo ya pwani wanashauriwa kuchukua tahadhari.


Hakuna maoni: