Breaking


Alhamisi, 29 Januari 2026

TFF YAUFUNGIA UWANJA WA KMC KWA MICHUANO YA LIGI KUKOSA VIGEZO

Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limeufungia Uwanja wa KMC, Dar es Salaam, kwa ajili ya michezo ya Ligi baada ya kugundua kwamba haukidhi vigezo vya kikanuni vilivyowekwa katika Kanuni za Leseni za Klabu.


TFF imesema kuwa miundombinu ya uwanja huo haikidhi matakwa yanayohitajika kisheria na kikanuni, ikiwemo masharti ya usalama na viwango vya ubora vinavyotakiwa kwa viwanja vinavyotumika katika mashindano rasmi.


Kwa mujibu wa uamuzi huu, timu zinazotumia Uwanja wa KMC kama uwanja wao wa nyumbani zitalazimika kucheza michezo yao kwenye viwanja vingine hadi pale ambapo uwanja huo utakaporidhiwa na TFF baada ya kufanyiwa maboresho na ukaguzi rasmi.


TFF pia imezikumbusha klabu zote nchini kuendelea kutunza na kuboresha miundombinu ya viwanja vyao ili kuepuka usitishaji wa michezo au vikwazo vya kikanuni.


Cliford Mario Ndimbo

Ofisa Habari na Mawasiliano, TFF

Januari 29, 2026


Hakuna maoni: