Breaking


Alhamisi, 15 Januari 2026

UCHAGUZI UGANDA LEO: MAANDALIZI YAKAMILIKA, HOFU YABAKI SIKU YA KURA




Maandalizi ya siku ya upigaji kura nchini Uganda yamekamilika, huku vifaa vya kupigia kura na mahitaji mengine muhimu vikisambazwa katika vituo mbalimbali vya usambazaji jana. Vifaa hivyo vinatarajiwa kufikishwa mapema asubuhi leo katika vituo vya kupigia kura kote nchini.


Mawakala wa vyama vya siasa na wagombea walikuwepo katika vituo vya usambazaji kusimamia na kuthibitisha uhalali na ubora wa vifaa, kama inavyotakiwa kisheria. Katika vituo vilivyotembelewa na BBC, mawakala walieleza kuridhishwa kwao na hali ya vifaa, wakisema viko katika viwango vinavyokubalika.


Hata hivyo, walionya kuwa wasiwasi wao mkubwa bado upo kuhusu mwenendo wa siku ya leo, ambapo raia wanatarajiwa kwenda debeni kutoa maamuzi yao. Baadhi yao walilalamikia hatua ya kuzimwa kwa huduma za mtandao, wakisema imeathiri mawasiliano na uratibu wa kazi zao.


Kwa upande mwingine, maafisa wa upigaji kura walitumia siku ya jana kujiandaa kwa mapokezi ya vifaa, ikiwa ni pamoja na kufanya mazoezi ya kuiga mchakato wa upigaji kura, ili kuhakikisha wanauelewa kikamilifu na kuutekeleza kwa usahihi siku ya leo.


Hakuna maoni: