Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imetangaza utabiri wa hali ya hewa kwa saa 24 zijazo kuanzia saa 3:00 usiku wa leo.
Kwa mujibu wa TMA, mikoa ya Rukwa, Kigoma, Tabora, Katavi, Kagera, Geita, Mwanza, Mara, Simiyu na Shinyanga inatarajiwa kupata hali ya mawingu kiasi, mvua na ngurumo katika maeneo machache pamoja na vipindi vya jua.
Mikoa ya Dodoma, Singida, Ruvuma, Songwe, Mbeya, Iringa na Njombe itakuwa na mawingu kiasi, mvua katika baadhi ya maeneo na vipindi vya jua.
Kwa Lindi na Mtwara, kunatarajiwa mawingu kiasi, mvua nyepesi na vipindi vya jua.
Hali ya mawingu kiasi na vipindi vya jua inatarajiwa katika Unguja na Pemba, pamoja na mikoa ya Arusha, Manyara, Kilimanjaro, Morogoro, Tanga, Dar es Salaam na Pwani ikiwemo Mafia.

Hakuna maoni:
Chapisha Maoni