Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imetoa utabiri wa hali ya hewa kwa saa 24 zijazo kuanzia saa 3:00 usiku wa leo, ikionesha mchanganyiko wa mawingu, mvua na vipindi vya jua katika mikoa mbalimbali nchini.
Kwa mujibu wa TMA, mvua na ngurumo zinatarajiwa katika mikoa ya Rukwa, Kigoma, Tabora na Katavi, huku mawingu kiasi na mvua za hapa na pale zikitarajiwa katika mikoa ya Ruvuma, Songwe, Mbeya, Iringa, Njombe, Morogoro, Tanga, Dar es Salaam, Pwani, Dodoma na Singida.
Aidha, hali ya mawingu kiasi na vipindi vya jua inatarajiwa katika mikoa ya Arusha, Manyara, Kilimanjaro, pamoja na Visiwa vya Unguja na Pemba.
TMA imewataka wananchi kuchukua tahadhari na kuendelea kufuatilia taarifa rasmi za hali ya hewa.

Hakuna maoni:
Chapisha Maoni