Breaking


Ijumaa, 16 Januari 2026

UTABIRI WA HALI YA HEWA KWA SAA 24 ZIJAZO

 



Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imetoa utabiri wa hali ya hewa kwa saa 24 zijazo kuanzia saa 3:00 usiku wa leo, ikieleza mwenendo wa hali ya hewa katika mikoa mbalimbali nchini.


Kwa mujibu wa TMA, mikoa ya Rukwa, Kigoma, Tabora na Katavi, pamoja na kusini mwa Mkoa wa Morogoro, inatarajiwa kuwa na hali ya mawingu kiasi huku mvua ikinyesha katika maeneo machache, ikifuatana na ngurumo za radi kwa nyakati tofauti.


Aidha, mikoa ya Kagera, Geita, Mwanza na Shinyanga, pamoja na mikoa ya Ruvuma, Songwe, Mbeya, Iringa na Njombe, inatarajiwa kushuhudia mvua za vipindi katika baadhi ya maeneo, zikiambatana na ngurumo za radi.


Kwa upande wa mikoa ya Dodoma na Singida, hali ya hewa inatarajiwa kuwa ya mawingu kiasi, huku mvua ikinyesha katika maeneo machache na vipindi vya jua kujitokeza.


TMA pia imesema kuwa mikoa ya Mara na Simiyu, Visiwa vya Unguja na Pemba, kaskazini mwa Mkoa wa Morogoro, pamoja na mikoa ya Arusha, Manyara na Kilimanjaro, itakuwa na hali ya mawingu kiasi na vipindi vya jua.


Vilevile, Mkoa wa Pwani ikijumuisha Visiwa vya Mafia, pamoja na mikoa ya Lindi, Mtwara, Tanga na Dar es Salaam, inatarajiwa kuwa na hali ya mawingu kiasi ikichanganyika na vipindi vya jua katika maeneo mengi.


Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania imewataka wananchi kuendelea kufuatilia taarifa rasmi za hali ya hewa na kuchukua tahadhari zinazostahili kulingana na mwenendo wa hali ya hewa katika maeneo yao.


Hakuna maoni: