Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Mkoani Dar es salaam, Edward Mpogolo, anawatangazia wananchi wote tume ya Uchunguzi ya matukio yaliyotokea wakati na baada ya uchaguzi Mkuu Oktoba 29 mwaka 2025 itakuwa Ilala January 19 Mwaka 2026.
Taarifa iliyotolewa na ofisi ya Mkuu wa wilaya ya Ilala, Edward Mpogolo, imeeleza tume hiyo itakutana na kuwasikiliza wananchi wa wilaya hiyo walioathirika na kufiwa na ndugu, kujeruhiwa na kuharibiwa na kuibiwa mali zao.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Mkuu wa wilaya ya Ilala, Edward Mpogolo, tume hiyo itakutana na wananchi hao siku ya jumatatu tarehe 19 January 2026, kuanzia saa tatu asubuhi, katika ukumbi wa Karimjee.
Mkuu wa wilaya ya Ilala, Edward Mpogolo, anawakaribisha wananchi wote walioguswa na matukio taja katika taarifa iliyotolewa.

Hakuna maoni:
Chapisha Maoni