Nchi kadhaa washirika wa Venezuela ikiwemo Urusi, Mexico na Brazil, zimelaani mashambulizi ya Marekani dhidi ya Venezuela.
Wizara ya Mambo ya Nje ya Urusi, imesema ni muhimu kuzuia kuongezeka kwa mgogoro huo na kutafuta mazungumzo na kwamba Urusi iko tayari kuchukua jukumu lenye kujenga.
Rais wa Brazil, Luiz Inacio Lula da Silva naye pia amelaani mashambulizi hayo akiyaita tishio kubwa kwa uhuru wa taifa hilo, na kuunga mkono wito kama huo uliotolewa na taifa jingine lenye ushawishi wa kikanda, Mexico.
Cuba, Iran, Argentina na Colombia pia nazo zimetoa wito wa kulaani mashambulizi hayo.
Nchi kadhaa za Umoja wa Ulaya zimesema zinafuatilia kwa ukaribu matukio ya Venezuela, huku Ujerumani ikielezea wasiwasi mkubwa.

Hakuna maoni:
Chapisha Maoni