Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Balozi Dkt. Bashiru Ally Kakurwa leo Januari 27, 2026, amekutana na timu ya wataalam wa wizara hiyo waliokuwa wanafanya usanifu wa ujenzi wa Kiwanda cha Kuchakata Samaki Wilayani Kilwa Mkoani Lindi, kitakachojengwa na Shirika la Uvuvi Tanzania (TAFICO) na kupokea taarifa ya usanifu wa ujenzi huo.
Kikao hicho kilichofanyika Ofisi ndogo ya Wizara iliyopo Kambarage Tower Jijini Dodoma, Pamoja na mambo mengine Mhe. Balozi Dkt. Bashiru ameiagiza timu hiyo kuongeza kasi ya utekelezaji wa ujenzi huo ili Kiwanda hicho kikamilike kwa wakati na kianze kuwanufaisha wananchi hususani wadau wa sekta ya uvuvi.





Hakuna maoni:
Chapisha Maoni